Mwanzo 5:18-32
Mwanzo 5:18-32 SRUV
Yaredi akaishi miaka mia moja na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Yaredi ni miaka mia tisa na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Methusela akaishi miaka mia moja na themanini na saba, akamzaa Lameki. Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Methusela ni miaka mia tisa na sitini na tisa, akafa. Lameki akaishi miaka mia moja na themanini na miwili, akazaa mwana. Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia tano na tisini na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. Baada ya Nuhu kufikisha umri wa miaka mia tano, aliwazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.