Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 5:18-32

Mwa 5:18-32 SUV

Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa. Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.