Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 42

42
Ndugu zake Yusufu waenda Misri
1 # Mdo 7:12 Basi Yakobo akaona ya kuwa kuna nafaka katika Misri, Yakobo akawaambia wanawe, Kwa nini mnatazamana? 2#Mwa 43:8; Zab 33:18,19; Isa 38:1 Akasema, Angalia, nimesikia ya kuwa kuna nafaka Misri; shukeni huko mkatununulie chakula, tupate kuishi wala tusife. 3Basi ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri ili wanunue nafaka. 4#Mwa 42:38 Lakini Benyamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumpeleka pamoja na ndugu zake, maana alisema, Mabaya yasimpate.
5 # Mwa 12:10; 26:1; Mdo 7:11 Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula miongoni mwao waliokuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani. 6#Mwa 41:41; 27:29; 33:6; 37:7; Rut 2:10; 1 Fal 1:16; Isa 60:14 Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake. 7Yusufu akawaona nduguze, akawatambua, lakini alijifanya kama mgeni kwao. Akasema nao kwa maneno makali, akawaambia, Mmetoka wapi ninyi? Wakasema. Tumetoka nchi ya Kanaani, ili tununue chakula. 8Yusufu akawatambua nduguze, bali wao hawakumtambua yeye. 9#Mwa 37:5-10 Yusufu akazikumbuka zile ndoto alizowaotea. Akawaambia, Wapelelezi ninyi, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi. 10Wakamwambia, Hasha, bwana, watumwa wako tumekuja ili tununue chakula. 11Sisi sote ni wana wa mtu mmoja tu watu wa kweli sisi; watumwa wako si wapelelezi. 12Akawaambia, Sivyo, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi. 13#Mwa 37:30; 44:20; Omb 5:7 Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
14Yusufu akawaambia, Ndivyo nilivyowaambia, nikisema, Wapelelezi ninyi. 15#1 Sam 1:26; 17:55 Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo. 16Mtumeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa jela, hadi maneno yenu yahakikishwe kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao hakika ninyi ni wapelelezi. 17Akawatia wote gerezani siku tatu. 18#Law 25:43; Neh 5:15 Siku ya tatu, Yusufu akawaambia, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi namcha Mungu. 19Kama ninyi ni wa kweli, mmoja wenu na afungwe gerezani, nanyi mwende mkachukue nafaka kwa ajili ya njaa ya nyumba zenu, 20#Mwa 43:5; 44:23 mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya. 21#Ayu 36:8,9; Hos 5:15; Zab 107:17; Mit 5:22; 11:21; Mt 7:2 Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata. 22#Mwa 9:5; 37:21-22; 1 Fal 2:32; 2 Nya 24:22; Zab 9:12; Lk 11:50,51 Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, Msimkosee kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo tunadaiwa damu yake. 23Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alizungumza nao kupitia kwa mkalimani. 24Akaenda kando, akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.
25 # Mt 5:44; Rum 12:17-21; 1 Pet 3:9 Yusufu akaamuru kuvijaza vyombo vyao nafaka, na kumrudishia kila mtu fedha yake katika gunia lake, na kuwapa chakula cha njiani. Na hivyo ndivyo walivyofanyiwa.
Ndugu zake Yusufu warudi Kanaani
26Wakawatwika punda wao nafaka yao, wakatoka huko. 27#Mwa 43:21 Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake. 28Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, Ni nini hii Mungu aliyotutendea?
29Wakaja kwa Yakobo, baba yao, katika nchi ya Kanaani, wakampasha habari za yote yaliyowapata, wakisema, 30#Mwa 42:7 Mtu yule aliye bwana wa nchi alisema nasi kwa maneno makali, akatufanya tu wapelelezi wa nchi. 31Tukamwambia, Tu watu wa kweli sisi, wala si wapelelezi. 32Sisi tu ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayuko, na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo katika nchi ya Kanaani. 33#Mwa 42:15,19,20 Yule mtu, bwana wa nchi, akatuambia, Kwa njia hii nitawajua kama ninyi ni watu wa kweli; ndugu yenu mmoja mwacheni huku kwangu, kachukueni nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mwende zenu. 34#Mwa 34:10 Mkaniletee ndugu yenu mdogo; ndipo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi, bali ni watu wa kweli; basi nitawarudishia ndugu yenu, nanyi mtafanya biashara katika nchi hii. 35#Mwa 43:21 Ikawa walipomimina magunia yao, kumbe! Bahasha ya fedha ya kila mtu imo katika gunia lake. Nao walipoziona bahasha za fedha zao, wao na baba yao waliogopa. 36#Mwa 43:14 Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi.
37Reubeni akamwambia baba yake, akasema, Uwaue wanangu wawili nisipomrudisha kwako; mtie katika mikono yangu, nami nitamrudisha kwako. 38#Mwa 37:33; 44:28-31 Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 42: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha