Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 35:16-29

Mwanzo 35:16-29 SRUV

Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali. Ikawa alipokuwa anashikwa sana na uchungu, mkunga akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu. Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo. Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi. Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili. Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni. Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu. Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka. Siku za Isaka zilikuwa miaka mia moja na themanini. Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Soma Mwanzo 35