Mwanzo 11:11-32
Mwanzo 11:11-32 SRUV
Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu. Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Nahori akaishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.