Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 11:11-32

Mwanzo 11:11-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. Hawa ndio wazao wa Tera. Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.

Shirikisha
Soma Mwanzo 11

Mwanzo 11:11-32 Biblia Habari Njema (BHN)

Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Arfaksadi alipokuwa na umri wa miaka 35, alimzaa Shela. Baada ya kumzaa Shela, Arfaksadi aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Shela alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Eberi. Baada ya kumzaa Eberi, Shela aliishi miaka 403 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Eberi alipokuwa na umri wa miaka 34, alimzaa Pelegi. Baada ya kumzaa Pelegi, Eberi aliishi miaka 430 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Pelegi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Reu. Baada ya kumzaa Reu, Pelegi aliishi miaka 209 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Reu alipokuwa na umri wa miaka 32, alimzaa Serugi. Baada ya kumzaa Serugi, Reu aliishi miaka 207 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Serugi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Nahori. Baada ya kumzaa Nahori, Serugi aliishi miaka 200 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Nahori alipokuwa na umri wa miaka 29, alimzaa Tera. Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka 119, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani. Wafuatao ni wazawa wa Tera, baba yao Abramu, Nahori na Harani. Harani alikuwa baba yake Loti. Huyo Harani alifariki wakati Tera baba yake alikuwa anaishi huko Uri alikokuwa amezaliwa. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai. Mke wa Nahori aliitwa Milka, binti Harani ambaye pia alikuwa baba yake Iska. Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa. Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205.

Shirikisha
Soma Mwanzo 11

Mwanzo 11:11-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu. Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Nahori akaishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.

Shirikisha
Soma Mwanzo 11

Mwanzo 11:11-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake. Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake. Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake. Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu. Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake. Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na wake. Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, waume na wake. Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.

Shirikisha
Soma Mwanzo 11