Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 23:10-12

Kutoka 23:10-12 SRUV

Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kupata mavuno yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni. Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.

Soma Kutoka 23

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 23:10-12