Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 13

13
Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu
1BWANA akasema na Musa, akamwambia, 2#Hes 3:13; 8:16; 18:15; Lk 2:23; Kut 22:29,30; Law 27:26; Kum 15:19 Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
3 # Kut 12:42; Kum 16:3; Kut 6:1 Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa. 4#Kut 23:15; 34:18; Kum 16:1 Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu. 5Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu. 6#Kut 12:15,16 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba, nayo siku ya saba itakuwa ni sikukuu ya BWANA. 7Mikate isiyochachwa italiwa katika hizo siku saba; mkate uliotiwa chachu usionekane kwako, wala chachu isionekane kwako, ndani ya mipaka yako yote. 8#Zab 44:1 Nawe utamwambia mwanao siku hiyo, ukisema, Ni kwa sababu ya hayo BWANA aliyonifanyia hapo nilipotoka Misri. 9#Kut 12:14; Hes 15:39; Kum 6:8; 11:18; Isa 49:16; Yer 22:24; Mt 23:5 Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. 10Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.
Kuweka wakfu mzaliwa wa kwanza
11 # Mwa 15:18; 17:8; Zab 105:42-45 Itakuwa hapo BWANA atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa, 12#Kut 34:19-20; Lk 2:23; Kut 22:29; Law 27:26; Hes 18:15; Eze 44:30 ndipo utamwekea BWANA kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao wa kiume watakuwa ni wa BWANA. 13#Hes 3:46 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; na kama hutaki kumkomboa, utamwua;#13:13 Katika Kiebrania ni: kuvunja shingo. na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. 14#Kut 12:26; Kum 6:20; Yos 4:6,21 Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa wa kiume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa. 16#Kum 6:8 Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
Nguzo za wingu na moto
17 # Kut 14:11; Hes 14:1; Kum 17:16 Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri; 18#Kut 11:2; Hes 33:6 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu;#13:18 Katika Kiebrania ni kuelekea Bahari ya Mafunjo. wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri wakiwa tayari kwa vita. 19#Mwa 50:25; Yos 24:32; Mdo 7:16 Musa akaichukua ile mifupa ya Yusufu pamoja naye; maana, alikuwa amewaapisha sana wana wa Israeli, akisema, Mungu hana budi atawajia ninyi; nanyi mtaichukua mfupa yangu kutoka hapa pamoja nanyi. 20#Hes 33:6 Nao wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpaka wa lile jangwa. 21#Kum 1:33; Neh 9:12,19; Zab 78:14; Isa 4:5; 1 Kor 10:1 BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku; 22#Zab 121:5-8 ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha