Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 27:1-10

Kumbukumbu la Torati 27:1-10 SRUV

Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza wale watu wakawaambia, Shikeni maagizo yote niwaagizayo leo. Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo BWANA, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo, uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako. Na iwe, mtakapokwisha vuka Yordani myasimamishe mawe haya, niwaagizayo hivi leo, katika mlima Ebali, nawe yatalize matalizo. Na huko umjengee madhabahu BWANA, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake. Jenga hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee BWANA, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake; ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako. Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana. Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako. Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.