Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 27:1-10

Kumbukumbu 27:1-10 NENO

Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi anayowapa BWANA Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na myapake chokaa. Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi anayowapa BWANA Mungu wenu, nchi inayotiririka maziwa na asali, kama vile BWANA, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, na myapake chokaa. Huko mjengeeni BWANA Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake. Jengeni madhabahu ya BWANA Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa BWANA Mungu wenu. Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za BWANA Mungu wenu. Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.” Kisha Musa na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la BWANA Mungu wako. Mtii BWANA Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”