Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo 4:9-18

2 Timotheo 4:9-18 SRUV

Jitahidi uwezavyo kuja kwangu upesi. Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. Lakini Tikiko nilimtuma Efeso. Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. Iskanda, mfua shaba, alionesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. Katika utetezi wangu wa kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Timotheo 4:9-18

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha