Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo 4

4
1 # Mdo 10:42; 1 Pet 4:5; Rum 14:9,10 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2#Mdo 20:20,31 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3#2 Tim 1:13; 1 Tim 4:1 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajikusanyia waalimu wengi, watakaowaambia yale tu masikio yao yanataka kusikia; 4#1 Tim 4:7; 2 The 2:11 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5#2 Tim 2:3; Efe 4:11 Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza huduma yako kwa ukamilifu. 6#Flp 2:17 Kwa maana, mimi sasa namiminwa kama tambiko, na wakati wa kuondoka kwangu umefika. 7#1 Kor 9:25; 1 Tim 6:12; Flp 3:14 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8#2 Tim 2:5; Yn 1:22; 1 Pet 5:4; Ufu 2:10 baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Maagizo binafsi
9 # 2 Tim 1:4 Jitahidi uwezavyo kuja kwangu upesi. 10#2 Kor 8:23; Gal 2:3; Kol 4:14; Tit 1:4; Flm 1:24 Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. 11#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; Kol 4:10,14; Flm 1:24 Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. 12#Mdo 20:4; Efe 6:21-22; Kol 4:7-8 Lakini Tikiko nilimtuma Efeso. 13#Mdo 20:6 Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. 14#Zab 28:4; 62:12; Mit 24:12; Rum 2:6; 1 Tim 1:20; 2 Sam 3:39 Iskanda, mfua shaba, alionesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa kulingana na matendo yake. 15Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. 16#2 Tim 1:15 Katika utetezi wangu wa kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17#Zab 22:21; Dan 6:21,28; Mdo 23:11; 27:23 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba. 18Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
Salamu za mwisho na baraka
19 # Mdo 18:2; 2 Tim 1:16-17 Nisalimie Priska na Akila, na wale wa nyumbani mwa Onesiforo. 20#Mdo 19:22; 20:4; 21:29; Rum 16:23 Erasto alibaki Korintho. Trofimo nilimwacha huku Mileto, mgonjwa. 21Jitahidi uwezavyo kuja kabla ya majira ya baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.
22Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi.

Iliyochaguliwa sasa

2 Timotheo 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha