Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 23

23
Maneno ya mwisho ya Daudi
1Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi.
Daudi, mwana wa Yese, anena,
Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu,
Yeye, masihi#23:1 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wake Mungu wa Yakobo,
Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;
2 # 2 Pet 1:21 Roho ya BWANA ilinena ndani yangu,
Na neno lake likawa ulimini mwangu.
3 # Kut 18:21 Mungu wa Israeli alisema,
Mwamba wa Israeli aliniambia,
Atawalaye wanadamu kwa haki,
Akitawala katika kicho cha Mungu,
4 # Mit 4:18 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,
Asubuhi isiyo na mawingu.
Likichipuza mimea ardhini,
Kwa mwangaza baada ya mvua;
5 # 1 Fal 9:4-6 Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA?
Kwa kuwa amefanya nami agano la milele;
Ina taratibu katika yote, ni thabiti,
Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
6Lakini hatawachipuza watu wasiofaa;
Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa,
Maana haichukuliki kwa mkono,
7Mtu atakayeigusa hiyo,
Na awe na chuma na mpini wa mkuki,
Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.
Mashujaa wa Daudi
8Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu#23:8 Au, Yosheb-bashebethi. Mhakmoni, Hamkuu wa wakuu wa majeshi; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja. 9#1 Nya 11:12; 27:4 Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 10huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. 11#1 Nya 11:12 Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo shamba lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; 12ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
13 # 1 Nya 11:15; 14:9; Kum 33:29; 1 Sam 22:1; 1 Nya 29:11; 2 Nya 14:11-14; 25:8; Zab 3:8; 46:1; Mit 21:30,31; Rum 8:31; 2 Sam 5:18; Isa 17:5 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. 14#1 Sam 22:4; 1 Nya 12:16 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. 15Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 16Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilichokuwa karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; lakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA. 17#Law 17:10 Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
18 # 2 Sam 2:18; 1 Nya 11:20 Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu. 19Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa kamanda wao; ila hakuweza kuwa kama wale watatu. 20#Yos 15:21; Kut 15:15 Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wawili wakali wa Moabu,#23:20 Au, wana wawili wa Arieli, wa Moabu. pia aliingia katika shimo na kumwua simba wakati wa theluji; 21#1 Nya 11:23 huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyang'anya Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 22Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 23#2 Sam 8:18 Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamteua kuwa mkuu wa walinzi wake.
24 # 2 Sam 2:18 Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu; 25#1 Nya 11:27 na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi; 26na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; 27na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi; 28na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi; 29na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini; 30#Amu 12:15; 2:9 na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi; 31na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi; 32na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani, 33mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari; 34na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni; 35na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi; 36na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi; 37na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; 38#2 Sam 20:26; Yos 15:48 na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri; 39#2 Sam 11:3,6 na Uria, Mhiti; idadi yao ilikuwa watu thelathini na saba.

Iliyochaguliwa sasa

2 Samweli 23: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha