Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wafalme 21

21
Manase atawala Yuda
1 # Isa 62:4 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba. 2#2 Fal 16:3 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli. 3#2 Fal 18:4; 1 Fal 16:32; Kum 4:19; 17:3; 2 Fal 17:16 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. 4#Yer 32:34; 2 Sam 7:13; 1 Fal 8:29; 9:3 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya BWANA, napo ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu. 5Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya BWANA. 6#Law 18:21; 20:2; 2 Fal 16:3; 17:17; 2 Nya 28:3; 33:6; Law 19:26,31; Kum 18:10 Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha. 7#1 Fal 8:29; 9:3; 2 Fal 23:27; Zab 132:13,14; Yer 32:34 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo BWANA alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; 8wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa. 9#1 Fal 14:16; 2 Nya 33:9; Mit 29:12 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa BWANA aliowaharibu mbele za wana wa Israeli. 10BWANA akanena kwa watumishi wake manabii, akisema, 11#2 Fal 23:26; 24:3,4; Yer 15:4; 1 Fal 21:26; Eze 16:3,45; 1 Pet 4:3; Ufu 21:8 Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake; 12#1 Sam 3:11; Yer 19:3 kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili. 13#Isa 34:11; Omb 2:8; Amo 7:7,8 Nami nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya Samaria, na timazi ya nyumba ya Ahabu; nami nitaifuta Yerusalemu, kama mtu afutavyo sahani, kuifuta na kuifudikiza. 14#2 Fal 19:30 Nami nitawatupa mabaki ya urithi wangu, na kuwatia mikononi mwa adui zao; nao watakuwa nyara na mateka kwa adui zao wote; 15kwa sababu wametenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha, tangu siku ile walipotoka baba zao katika Misri, hata leo hivi. 16#Mwa 9:6; 2 Fal 24:4; Zab 10:2,8; 106:38; Mit 6:16,17; Isa 59:3,7; Yer 2:34; 19:3,4; Omb 4:13,14; Eze 9:9; 22:1-27; Mik 3:9-12; Yoe 3:19 Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa BWANA. 17#2 Nya 33:11-19 Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? 18#Yer 22:19; 2 Nya 33:20 Manase akalala na babaze, akazikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, yaani, bustani ya Uza. Na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.
Amoni atawala Yuda
19 # 2 Nya 33:21-23 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka miwili huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Meshulemethi, binti Haruzi wa Yotba. 20Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kama Manase babaye alivyofanya. 21Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu. 22#Kum 32:15; Amu 2:12; 1 Fal 11:33 Akamwacha BWANA, Mungu wa babaze, wala hakuiendea njia ya BWANA. 23#2 Fal 12:20; 14:19; 2 Nya 33:24,25 Nao watumishi wa Amoni wakamfitinia, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe. 24Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfitinia mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake. 25Basi mambo yote ya Amoni yaliyosalia, aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? 26#Mt 1:10 Akazikwa kaburini mwake katika bustani ya Uza. Na Yosia mwanawe akatawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wafalme 21: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia