Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wafalme 20

20
Kuugua kwa Hezekia
1 # 2 Nya 32:24; Isa 38:1; 2 Sam 17:23 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 2Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA akasema, 3#Neh 13:22; Zab 132:1-5; Isa 38:3; Mwa 5:22,24; 17:1; 1 Fal 3:6 Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. 4Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema, 5#1 Fal 18:37; 2 Fal 19:20; 2 Nya 32:20,21; Zab 65:2; 69:18,19; Lk 11:9,10; Mdo 10:31; Ayu 16:20; Zab 39:12; 56:8; Ufu 7:17 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA. 6#2 Fal 19:34; 2 Nya 32:22 Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu. 7Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona. 8Hezekia akamwambia Isaya, Je! Kutakuwa na ishara gani ya kwamba BWANA ataniponya, nami siku ya tatu nitapanda nyumbani kwa BWANA. 9#Isa 38:7 Isaya akamwambia, Jambo hili litakuwa ishara kwako, itokayo kwa BWANA, ya kwamba BWANA atalifanya neno hilo alilolinena; je! Kivuli kiendelee madaraja kumi, au kirudi nyuma madaraja kumi? 10Hezekia akajibu, Ni jambo jepesi kivuli kuendelea madaraja kumi; la, hicho kivuli na kirudi nyuma madaraja kumi. 11#Yos 10:12-14; 2 Nya 32:24,31; Isa 38:8 Isaya nabii akamlilia BWANA; akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, ambayo kilikuwa kimeshuka katika madaraja ya Ahazi.
Wajumbe kutoka Babeli
12 # Isa 39:1 Wakati huo Merodak-baladani mwana wa Baladani, Mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana alipata habari kwamba Hezekia ameugua. 13#2 Nya 32:27,31 Hezekia akawasikiliza, akawaonesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote. 14Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Wasemaje watu hawa? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, yaani Babeli. 15Ndipo akasema, Wameona nini nyumbani mwako? Hezekia akajibu, Vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu wameviona; hapana kitu nisichowaonesha katika hazina zangu. 16Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la BWANA, 17#Law 26:33; 2 Fal 24:13; Yer 27:21; 52:17 Angalia, siku zinakuja, ambazo vitu vyote vilivyomo nyumbani mwako, na hivyo vilivyowekwa akiba na baba zako hata leo, vitachukuliwa mpaka Babeli; hakitasalia kitu, asema BWANA. 18#2 Fal 24:12,14; Dan 1:3 Na baadhi ya wanao watakaotoka kwako, utakaowazaa, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi jumbani mwake mfalme wa Babeli. 19#1 Sam 3:18; Ayu 1:21; Zab 39:9; Omb 3:22,39 Ndipo Hezekia akamwambia Isaya, Neno la BWANA ulilolinena ni jema. Tena akasema, Je! Sivyo, ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?
Kifo cha Hezekia
20 # Neh 3:16 Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? 21Hezekia akalala na baba zake; na Manase mwanawe akatawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wafalme 20: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia