2 Wakorintho 6:11-13
2 Wakorintho 6:11-13 SRUV
Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.