2 Mambo ya Nyakati UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu hiki kinaendeleza masimulizi ya Kitabu cha Kwanza, kikianzia pale cha Kwanza kilipomalizika. Mwandishi anaanza na habari za Solomoni na jambo kubwa kwake ni ujenzi wa hekalu. Ufalme wa Kaskazini haushughulikiwi kwa kuwa uongozi wake hautokani na nasaba ya Daudi. Mtawala anayesifiwa ni yule aliyetokana na nasaba ya Daudi, akafuata mafundisho ya makuhani wa Kilawi. Mwandishi anaeleza kwa kirefu shughuli za matengenezo ya kidini hali shughuli za kisiasa zinaelezwa kwa kifupi.
Mwandishi anasimulia mitafaruku kati ya makabila ya Kaskazini na Kusini. Sehemu kubwa anaeleza Ufalme wa Kusini hadi mji wa Yerusalemu ulipoangamizwa. Mwandishi ana mkazo maalumu kuhusu taifa na dini. Heri ya Israeli ilitokana na Mungu: aidha ahadi za Mungu kwa Daudi zilitimilika, ikiwa watu walikuwa waaminifu kwa Agano, na kufuata mapenzi ya Mungu.
Yaliyomo:
1. Utawala wa mfalme Sulemani, Sura 1—8
(a) Kufaulu kwa Sulemani, (1)
(b) Kujenga hekalu na sanduku la Agano kuletwa hekaluni (2—7)
(c) Utukufu wa Sulemani (8—9)
2. Kugawanywa kwa Israeli, Sura 10
3. Wafalme wa Kusini inayoitwa Yuda, Sura 11:1—36:14
4. Kuangamizwa kwa Yerusalemu, Sura 36:15-21
5. Tangazo la Koreshi: Wayahudi kurudi na kujenga hekalu, Sura 36:22-23
Iliyochaguliwa sasa
2 Mambo ya Nyakati UTANGULIZI: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.