Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 1

1
Sulemani aomba hekima
1 # 1 Fal 2:46; Mwa 21:22; 39:2; 1 Nya 17:8; 29:25; Mt 28:20 Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alijiimarisha katika ufalme wake, naye BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno. 2#1 Nya 27:1; 2 Nya 29:20; 30:2 Sulemani akawaita Israeli wote, na makamanda wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila kiongozi wa Israeli, na wakuu wa familia. 3#1 Fal 3:4 Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo lilipokuwako hema la kukutania la Mungu, alilolifanya Musa mtumishi wa BWANA jangwani. 4#2 Sam 6:2; 1 Nya 15:1 Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu. 5#Kut 27:1; 38:1; 31:2 Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanya Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea. 6#1 Fal 3:4 Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu yake.
7 # 1 Fal 3:5; Mit 3:5; Isa 58:9 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. 8#1 Nya 28:5 Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. 9#1 Fal 3:7 Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. 10#1 Fal 3:9; Zab 119:34,73; Mit 3:13; Yak 1:5; Hes 27:17; Kum 31:2 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwatawala watu wako hawa walio wengi? 11#1 Sam 16:7; 1 Fal 3:11; 8:18 Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha ya wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwatawala watu wangu, niliokutawaza juu yao; 12#Zab 34:9,10; Mt 6:33; Efe 3:20; 1 Nya 29:25; 2 Nya 9:22; Mhu 2:9 basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo. 13Basi Sulemani akatoka mahali pa juu pa Gibeoni, toka mbele ya Hema la kukutania, akaja mpaka Yerusalemu; akatawala Israeli.
Shughuli za jeshi na biashara za mfalme Sulemani
14 # 1 Fal 4:26 Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu moja na mia nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 15#1 Fal 10:27; Ayu 22:24 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 16Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake. 17Nao walipandisha na kununua gari kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha; na farasi kwa mia moja na hamsini, vivyo hivyo wakawauzia wafalme wote Wahiti na wafalme wa Shamu.#1:17 Katika Kiebrania maana ya mstari huu sio dhahiri.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia