Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 17

17
Utawala wa Yehoshafati
1Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake, akajitia nguvu juu ya Israeli. 2#2 Nya 11:11; 15:8 Akaweka jeshi katika miji yote yenye maboma ya Yuda, akatia na askari walinzi katika nchi ya Yuda, na katika miji ya Efraimu, aliyoitwaa Asa babaye. 3#Rum 8:31 Naye BWANA alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute Mabaali; 4#Lk 1:6; 1 Fal 12:28 lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. 5#1 Sam 10:27; 1 Fal 10:25,27; 2 Nya 18:1 Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na watu wote wa Yuda; basi akawa na mali na heshima tele. 6#1 Fal 22:43; 2 Nya 14:3; 15:17; 19:3 Ukainuliwa moyo wake katika njia za BWANA; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na Maashera, katika Yuda. 7#2 Nya 15:3 Tena, katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, akawatuma wakuu wake, yaani, Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli, na Mikaya, ili kufundisha mijini mwa Yuda; 8na pamoja nao Walawi, yaani, Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adonia, Tobia, na Tob-adonia, Walawi; na pamoja nao Elishama na Yehoramu, makuhani. 9#2 Nya 35:3; Law 10:11; Neh 8:7; Mal 2:7 Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha Torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu. 10#Mwa 35:5; Kut 15:15; Kum 11:25; 2 Nya 14:14 Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati. 11#2 Sam 8:2 Na baadhi ya Wafilisti walimletea Yehoshafati zawadi, na fedha ya kodi; Waarabu nao wakamletea kondoo dume elfu saba na mia saba, na mabeberu elfu saba na mia saba. 12Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina. 13Naye alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda; na watu wa vita, watu mashujaa humo Yerusalemu. 14Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, makamanda wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa elfu mia tatu; 15na wa pili wake Yehohanani kamanda, na pamoja naye elfu mia mbili na themanini; 16#Amu 5:2,9; 1 Nya 29:9-17; Zab 110:3; 2 Kor 8:12 na baada yake Amasia mwana wa Zikri, aliyejitoa kwa BWANA kwa moyo, na pamoja naye elfu mia mbili, watu mashujaa; 17na wa Benyamini; Eliada mtu shujaa, na pamoja naye elfu mia mbili wenye nyuta na ngao; 18na wa pili wake Yehozabadi, na pamoja naye elfu mia moja na themanini waliojiweka tayari kwa vita. 19Hao ndio waliomngojea mfalme, zaidi ya hao mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika Yuda yote.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha