Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 16

16
Muungano na Aramu walaumiwa
1 # 1 Fal 15:17; 2 Nya 15:9 Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli alipanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda. 2Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema, 3Na pawepo agano la kushirikiana kati yangu na wewe kama lilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako; tazama, nimekutumia fedha na dhahabu; basi, uvunje mkataba wako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aache kunishambulia. 4Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma makamanda wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli; wakapiga Iyoni, na Dani, na Abel-maimu, na miji ya hazina yote ya Naftali. 5Baasha aliposikia habari hiyo, akaacha kuujenga Rama, akaifunga kazi yake. 6Ndipo mfalme Asa akawatwaa Yuda wote; nao wakayachukua mawe ya Rama, na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye akajenga kwa vitu hivyo Geba na Mispa.
7 # 1 Fal 16:1; 2 Nya 19:2; 20:34; Zab 146:3-6; Isa 31:1; Yer 17:5; Efe 1:12,13 Wakati huo Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea BWANA, Mungu wako, kwa hiyo limekutoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako. 8#2 Nya 14:9; 12:3 Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea BWANA, aliwatia mkononi mwako. 9#2 Nya 6:20; Ayu 34:21; Mit 5:21; 15:3; Yer 16:17; 32:19; Zek 4:10; Ebr 4:13; 1 Pet 3:12; 1 Sam 13:13; 1 Nya 21:8; Yer 5:21; Mt 5:22; 1 Kor 15:36; 1 Fal 15:32 Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita. 10#2 Nya 18:26; Yer 20:2; Mt 14:3 Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia katika nyumba ya magandalo gerezani, maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na wakati uleule Asa akatesa baadhi ya watu.
Ugonjwa na kifo cha mfalme Asa
11Na tazama, mambo yake Asa, toka mwanzo hadi mwisho, angalia, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 12#Kum 28:22; Yer 17:5 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada wa waganga. 13Asa akalala na babaze, akafa katika mwaka wa arubaini na mmoja wa kumiliki kwake. 14#Mwa 50:2; Mk 16:1 Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 16: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha