Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wathesalonike 5:21-28

1 Wathesalonike 5:21-28 SRUV

jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna. Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya. Ndugu, tuombeeni. Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.