1 Wathesalonike 5:21-28
1 Wathesalonike 5:21-28 NEN
Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. Jiepusheni na uovu wa kila namna. Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo. Ndugu, tuombeeni. Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen.