Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 4

4
Wazawa wa Yuda
1 # Mwa 38:29; 46:12; Hes 26:20,21; Rut 4:18 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. 2Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. 3Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na dada yao aliitwa jina lake Haselelponi; 4na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu. 5Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. 6Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. 7Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. 8Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu. 9#Mwa 34:19; Zab 112:6; Mit 10:7; Mwa 3:16 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni. 10#Mwa 12:8; 1 Nya 16:8; Ayu 12:4; 22:27; Isa 12:4; 1 Fal 3:7-13; Zab 21:4; 65:2; Mt 7:7-11 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
11Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni. 12Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka. 13#Yos 15:17 Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi na Meonothai.#4:13 Makala ya Kiebrania haina Meonothai. 14#Neh 11:35 Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu;#4:14 Maana yake ‘Bonde la Wahunzi’. kwani hao walikuwa mafundi stadi. 15Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi. 16Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli. 17Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa. 18Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa. 19Na wana wa mkewe Hodia, dada yake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka. 20Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.
21 # Mwa 38:1 Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa ukoo wa wafuma nguo za kitani safi, wa ukoo wa Ashbea; 22#2 Sam 8:2 na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. (Na taarifa hizi ni za zamani sana). 23Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
Wazawa wa Simeoni
24Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli; 25na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma. 26Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei. 27Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; lakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kama wana wa Yuda. 28Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali; 29na huko Bilha, na Esemu, na Toladi; 30na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi; 31na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hadi wakati wa kutawala kwa Daudi. 32Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano, 33na vijiji vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo. 34Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia; 35na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli; 36na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya; 37na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya; 38hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na koo za baba zao zikaongezeka sana. 39Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. 40#Mwa 9:22; 10:6; Zab 78:51 Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu. 41#2 Fal 18:8 Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao. 42Na baadhi yao, wana wa Simeoni wapatao watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi. 43#1 Sam 15:8; 30:17; 2 Sam 8:12 Nao wakawaua Waamaleki waliokuwa wamenusurika, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia