Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 3

3
Wazawa wa Daudi na Sulemani
1 # 1 Sam 25:43; 27:3; 2 Sam 3:2; Yos 15:56 Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli; 2wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi; 3#2 Sam 3:5 wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe. 4#2 Sam 2:11; 1 Fal 2:11; 2 Sam 5:5 Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akatawala miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 5#1 Nya 14:4; 2 Sam 12:24 Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu; 6na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti; 7na Noga, na Nefegi, na Yafia; 8#2 Sam 5:14 na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu tisa. 9#2 Sam 13:1; 14:27 Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa dada yao. 10#1 Fal 11:43; 14:31; 15:6 Na wazawa wa Sulemani walikuwa: Rehoboamu mwanawe; mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati; 11na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi; 12na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu; 13na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase; 14na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia. 15Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu. 16#Mt 1:11; 2 Fal 24:17 Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia. 17#Mt 1:12 Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, 18na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia. 19#Ezr 3:2 Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa dada yao; 20na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano. 21Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.#3:21 Au, hivi, Na wana wa Hanania; Pelatia, na mwanawe huyo ni Yeshaya, na mwanawe huyo ni Refaya, na mwanawe huyo ni Arnani, na mwanawe huyo ni Obadia, na mwanawe huyo ni Shekania. 22#Ezr 8:2 Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita. 23Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu. 24Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia