Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54 SRUV

Adamu, na Sethi, na Enoshi; na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki; na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Abrahamu. Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura. Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli. Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.