Wim 3
3
Ndoto za Mapenzi
1 #
Zab 4:6; 6:6; Isa 26:9 Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,
Nalimtafuta, nisimpate.
2Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,
Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.
Nikamtafuta, nisimpate.
3 #
Wim 5:7; Isa 21:6-8,11,12 Walinzi wazungukao mjini waliniona;
Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 #
Mit 8:17; 4:13; Rum 8:35,39 Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea,
Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;
Nikamshika, nisimwache tena,
Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,
Chumbani mwake aliyenizaa.
5 #
Wim 2:7
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
Bwana Arusi na Kundi lake Wakaribia
6 #
Wim 8:5; Yer 2:2 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,
Mfano wake ni nguzo za moshi;
Afukizwa manemane na ubani,
Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7Tazama, ni machela yake Sulemani;
Mashujaa sitini waizunguka,
Wa mashujaa wa Israeli.
8Wote wameshika upanga,
Wamehitimu kupigana;
Kila mtu anao upanga wake pajani
Kwa hofu ya kamsa za usiku.
9Mfalme Sulemani alijifanyizia machela
Ya miti ya Lebanoni;
10 #
Mt 22:37; Yn 13:1,34; Rum 5:8; Efe 3:19; 1 Pet 1:7,8 Nguzo zake alizifanyiza za fedha,
Na mgongo wake wa dhahabu,
Kiti chake kimepambwa urujuani,
Gari lake limenakishiwa njumu,
Hiba ya binti za Yerusalemu.
11 #
Ufu 11:15; Zab 110:3; Isa 62:5 Tokeni, enyi binti za Sayuni,
Mtazameni Mfalme Sulemani,
Amevaa taji alivyovikwa na mamaye,
Siku ya maposo yake,
Siku ya furaha ya moyo wake.
Iliyochaguliwa sasa
Wim 3: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.