Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wim 2

2
1Mimi ni ua la uwandani,#2:1Uwanda kwa Kiebrania ni Sharon.
Ni nyinyoro ya mabondeni.
2Kama nyinyoro kati ya miiba,
Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti.
3 # Mwa 3:6; Ufu 22:1 Kama mpera kati ya miti ya msituni,
Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana.
Naliketi kivulini mwake kwa furaha,
Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu.
4Akanileta mpaka nyumba ya karamu,
Na bendera yake juu yangu ni mapenzi.
5Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera,
Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
6 # Wim 8:3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
Nao wa kuume unanikumbatia!
7Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
8 # Yn 10:4 Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja,
Akiruka milimani, akichachawa vilimani.
9Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala.
Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu,
Achungulia dirishani, atazama kimiani.
10Mpendwa wangu alinena, akaniambia,
Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
11Maana tazama, kaskazi imepita,
Masika imekwisha, imekwenda zake;
12Maua yatokea katika nchi,
Wakati wa kupelea umefika,
Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
13Mtini wapevusha tini zake,
Na mizabibu inachanua,
Inatoa harufu yake nzuri;
Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
14 # Wim 8:13 Hua wangu, mafichoni mwa jabali,
Katika sitara za magenge,
Nitazame uso wako, nisikie sauti yako,
Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri.
15 # Zab 80:13; Eze 13:4; Lk 13:32 Tukamatie mbweha,
Wale mbweha wadogo,
Waiharibuo mizabibu,
Maana mizabibu yetu yachanua.
16 # Wim 6:3 Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake;
Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
17 # Wim 4:6; Lk 1:78; Rum 13:12; 2 Pet 1:19; Wim 8:14 Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,
Unigeukie, mpendwa wangu,
Nawe uwe kama paa, au ayala,
Juu ya milima ya Betheri.

Iliyochaguliwa sasa

Wim 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha