Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wim 3

3
Ndoto za Mapenzi
1 # Zab 4:6; 6:6; Isa 26:9 Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,
Nalimtafuta, nisimpate.
2Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,
Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.
Nikamtafuta, nisimpate.
3 # Wim 5:7; Isa 21:6-8,11,12 Walinzi wazungukao mjini waliniona;
Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 # Mit 8:17; 4:13; Rum 8:35,39 Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea,
Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;
Nikamshika, nisimwache tena,
Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,
Chumbani mwake aliyenizaa.
5 # Wim 2:7 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
Bwana Arusi na Kundi lake Wakaribia
6 # Wim 8:5; Yer 2:2 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,
Mfano wake ni nguzo za moshi;
Afukizwa manemane na ubani,
Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7Tazama, ni machela yake Sulemani;
Mashujaa sitini waizunguka,
Wa mashujaa wa Israeli.
8Wote wameshika upanga,
Wamehitimu kupigana;
Kila mtu anao upanga wake pajani
Kwa hofu ya kamsa za usiku.
9Mfalme Sulemani alijifanyizia machela
Ya miti ya Lebanoni;
10 # Mt 22:37; Yn 13:1,34; Rum 5:8; Efe 3:19; 1 Pet 1:7,8 Nguzo zake alizifanyiza za fedha,
Na mgongo wake wa dhahabu,
Kiti chake kimepambwa urujuani,
Gari lake limenakishiwa njumu,
Hiba ya binti za Yerusalemu.
11 # Ufu 11:15; Zab 110:3; Isa 62:5 Tokeni, enyi binti za Sayuni,
Mtazameni Mfalme Sulemani,
Amevaa taji alivyovikwa na mamaye,
Siku ya maposo yake,
Siku ya furaha ya moyo wake.

Iliyochaguliwa sasa

Wim 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha