Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 96

96
Sifa kwa Mungu atoaye Hukumu
1Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Mwimbieni BWANA, nchi yote.
2Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake,
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
3Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
4Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
5 # Isa 41:24; Yer 10:11; Hab 2:18-20; Mdo 19:26; 1 Kor 8:4,5; Mwa 1:1; Isa 42:5; Yer 10:11 Maana miungu yote ya watu si kitu,
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
6Heshima na adhama ziko mbele zake,
Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7 # Zab 29:1-2 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
8Mpeni BWANA utukufu wa jina lake,
Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.
9Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu,
Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
10 # Ufu 11:15; Yn 5:22 Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki;
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,
Atawahukumu watu kwa adili.
11Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,
Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
12Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;
13 # Ufu 19:11 Mbele za BWANA, kwa maana anakuja,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa uaminifu wake.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 96: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha