Zab 9:11-20
Zab 9:11-20 SUV
Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni, Yatangazeni kati ya watu matendo yake. Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka, Hakukisahau kilio cha wanyonge. Wewe, BWANA, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti, Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako. Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao. BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake. Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima; Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele. BWANA, usimame, mwanadamu asipate nguvu, Mataifa wahukumiwe mbele zako. BWANA, uwawekee kitisho, Mataifa na wajijue kuwa ni binadamu.