Zaburi 9:11-20
Zaburi 9:11-20 NEN
Mwimbieni BWANA sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa. Ee BWANA, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako. Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. BWANA anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. Ee BWANA, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako. Ee BWANA, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.