Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 22:1-19

Zab 22:1-19 SUV

Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao; Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu. Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi. Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, BWANA, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia.

Picha ya aya ya Zab 22:1-19

Zab 22:1-19 - Mungu wangu, Mungu wangu,
Mbona umeniacha?
Mbona U mbali na wokovu wangu,
Na maneno ya kuugua kwangu?
Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu
Na wakati wa usiku lakini sipati raha.
Na Wewe U Mtakatifu,
Uketiye juu ya sifa za Israeli.
Baba zetu walikutumaini Wewe,
Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.
Walikulilia Wewe wakaokoka,
Walikutumaini wasiaibike.
Lakini mimi ni mdudu wala si mtu,
Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.
Wote wanionao hunicheka sana,
Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;
Husema, Umtegemee BWANA; na amponye;
Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.
Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,
Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.
Kwako nalitupwa tangu tumboni,
Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.
Usiwe mbali nami maana taabu i karibu,
Kwa maana hakuna msaidizi.

Mafahali wengi wamenizunguka,
Walio hodari wa Bashani wamenisonga;
Wananifumbulia vinywa vyao,
Kama simba apapuraye na kunguruma.
Nimemwagika kama maji,
Mifupa yangu yote imeteguka,
Moyo wangu umekuwa kama nta,
Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu.
Nguvu zangu zimekauka kama gae,
Ulimi wangu waambatana na taya zangu;
Unaniweka katika mavumbi ya mauti
Kwa maana mbwa wamenizunguka;
Kusanyiko la waovu wamenisonga;
Wamenizua mikono na miguu.
Naweza kuihesabu mifupa yangu yote;
Wao wananitazama na kunikodolea macho.
Wanagawanya nguo zangu,
Na vazi langu wanalipigia kura.
Nawe, BWANA, usiwe mbali,
Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 22:1-19