Zab 119:1-10
Zab 119:1-10 SUV
Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake. Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.