Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:1-10

Zaburi 119:1-10 NEN

Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya BWANA. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote. Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa. BWANA Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.