Zab 105:1-11
Zab 105:1-11 SUV
Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake. Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka. Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele. Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa.