Mit 28:20-28
Mit 28:20-28 SUV
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate. Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia. Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake. Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA atawandishwa. Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.