Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 28:13-20

Mit 28:13-20 SUV

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara. Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini. Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake. Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.

Soma Mit 28

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 28:13-20