Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 14:1-35

Mit 14:1-35 SUV

Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi. Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu. Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa. Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki. Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa; Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake. Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai. Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa. Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki. Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi. Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri. Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema. Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Soma Mit 14

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 14:1-35