Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 14:1-35

Methali 14:1-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi. Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu. Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa. Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki. Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa; Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake. Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai. Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa. Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki. Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi. Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri. Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema. Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Shirikisha
Soma Methali 14

Methali 14:1-35 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Mwenye mwenendo mnyofu humcha Mwenyezi-Mungu, lakini mpotovu humdharau Mungu. Mpumbavu hujiadhibu mwenyewe kwa kuropoka kwake, lakini mwenye hekima hulindwa na maneno yake. Bila ng'ombe wa kulima ghala za mtu ni tupu, mavuno mengi hupatikana kwa nguvu ya ng'ombe wa kulima. Shahidi mwaminifu hasemi uongo, lakini asiyeaminika hububujika uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima bure, lakini mwenye busara hupata maarifa kwa urahisi. Ondoka mahali alipo mpumbavu, maana hapo alipo hamna maneno ya hekima. Hekima ya mwenye busara humwonesha njia yake, lakini upumbavu wa wapumbavu huwadanganya wenyewe. Wapumbavu huchekelea dhambi, bali wanyofu hupata fadhili kwa Mungu. Moyo waujua uchungu wake wenyewe, wala mgeni hawezi kushiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Njia unayodhani kuwa ni sawa, mwishoni yaweza kukuongoza kwenye kifo. Huzuni yaweza kufichika katika kicheko; baada ya furaha huja majonzi. Mtu mpotovu atavuna matunda ya mwenendo wake, naye mtu mwema atapata tuzo la matendo yake. Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari. Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu. Mwenye kuwaka hasira haraka hutenda kipumbavu, lakini mwenye busara ana uvumilivu. Wajinga hurithi upumbavu, lakini wenye busara hutuzwa taji ya maarifa. Waovu watapiga magoti mbele ya watu wema, watu wabaya mlangoni mwa waadilifu. Maskini huchukiwa hata na jirani yake, lakini tajiri ana marafiki wengi. Anayemdharau jirani yake ni mwenye dhambi, bali ana heri aliye mwema kwa maskini. Anayepanga maovu kweli anakosea! Wanaopanga kutenda mema hufadhiliwa. Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Mali ni taji ya fahari ya wenye hekima, lakini ujinga ni shada la wapumbavu. Shahidi wa kweli huokoa maisha, lakini msema uongo ni msaliti. Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuepa mitego ya kifo. Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia. Mtu asiye mwepesi wa hasira ana busara kubwa, lakini akasirikaye upesi hukuza upumbavu. Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Mwovu huangamizwa kwa matendo yake maovu, lakini mwadilifu hupata usalama kwa unyofu wake. Hekima imo moyoni mwa mtu mwenye busara; haipatikani kamwe mioyoni mwa wapumbavu. Uadilifu hukuza taifa, lakini dhambi ni balaa kwa taifa lolote. Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa.

Shirikisha
Soma Methali 14

Methali 14:1-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi. Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu. Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa. Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki. Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa; Bali hema la mwenye haki litafanikiwa. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake. Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali. Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa. Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki. Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana marafiki wengi. Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri. Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema. Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji la wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wowote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Shirikisha
Soma Methali 14

Methali 14:1-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha BWANA, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu, bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi. Shahidi mwaminifu hadanganyi, bali shahidi wa uongo humimina uongo. Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu. Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake. Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake. Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake. Mtu mwenye hekima humcha BWANA na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu, naye mtu wa hila huchukiwa. Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki. Maskini huepukwa hata na majirani zao, bali matajiri wana marafiki wengi. Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu. Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu. Yeye amchaye BWANA ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia. Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu. Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu. Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote. Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha.

Shirikisha
Soma Methali 14