Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 28

28
Sadaka za Kila Siku
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Law 3:11; 21:6,8; Mal 1:7,12Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao. 3#Kut 29:38Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsongezea BWANA; wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 4#Kut 12:6Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni; 5#Kut 16:36; 29:38-42; Law 2:1; Hes 15:4pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. 6Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto. 7#Kut 29:42; 30:9; Law 23:13; Hes 15:5-10; Isa 57:1Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia BWANA katika mahali hapo patakatifu. 8Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa BWANA.
Sadaka za Sabato
9Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji; 10#Eze 46:4hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Sadaka za Kila Siku
11 # Hes 10:10; 1 Sam 20:5; 1 Nya 23:31; 2 Nya 2:4; Ezr 3:5; Neh 10:33; Isa 1:13,14; Eze 45:17; Hos 2:11; Kol 2:16 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; 12#Hes 15:4; 29:10; Eze 46:5,7pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; 13na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 14Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng’ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Sadaka za Pasaka
16 # Kut 12:1-13; Kum 16:1-2; Law 23:5; Eze 45:21; Mt 26:2,17; Lk 22:7 Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya BWANA. 17#Kut 12:14-20; 23:15; 34:18; Kum 16:3-8; Law 23:6Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba. 18#Law 23:7Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 19#Law 22:20; Hes 29:8; Kum 15:21lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA; ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; 20pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume; 21na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba; 22#Law 16:18; Rum 8:3; Gal 4:4; Ebr 9:12; 10:1tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 23Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. 24#2 Kor 2:15; Efe 5:2Mtasongeza sadaka kwa mfano huu kila siku muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. 25#Kut 12:16; 13:6; Law 23:8Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi.
Sadaka za Majuma
26 # Kut 23:16; 34:22; Kum 16:9-12; Law 23:10,15; Mit 3:9; Mdo 2:1 Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsongezea BWANA sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 27#Law 23:18,19lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe waume wadogo wawili, kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; 28pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, 29na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba; 30na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 31Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 28: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia