Hes 27
27
Mabinti wa Selofehadi
1 #
Hes 14:35; 26:33; 36:1,11; 1 Nya 7:15; Yos 17:3 Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. 2#Hes 26:64,65; 14:22-37; Rum 5:12; 6:23Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema, 3Babaetu alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume cha BWANA katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe; naye alikuwa hana wana wa kiume. 4Kwa nini basi jina la babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu. 5#Kut 18:15; 25:22; Law 24:12,13; Mit 3:5,6Basi Musa akaleta neno lao mbele ya BWANA 6BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 7#Hes 36:2Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao. 8Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo utampa binti yake urithi wake. 9Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake. 10Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake. 11#Hes 35:29Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Yoshua Afanywa Kiongozi wa Waisraeli baada ya Musa
12 #
Kum 3:23-27; 32:48-52; 34:1 BWANA akamwambia Musa, Panda wewe juu ya mlima huu wa Abarimu, uitazame nchi niliyowapa wana wa Israeli. 13#Hes 20:24,28; 31:2; Kum 10:6; 32:50,52Na ukiisha kuiona, wewe nawe utakusanyika pamoja na baba zako, kama Haruni ndugu yako alivyokusanyika; 14#Kum 1:37; 32:51; Zab 106:32; Kut 17:7; Hes 20:1,13,24kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.) 15Musa akanena na BWANA akisema, 16#Hes 16:22; Ebr 12:9; Zek 12:1BWANA, Mungu wa roho za wenye mwili wote, na aweke mtu juu ya mkutano, 17#1 Fal 22:17; Eze 34:5; Mt 9:36; Mk 6:34; Kum 31:2; 1 Sam 8:20; 18:13; 2 Nya 1:10; 2 Nya 18:16atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa BWANA wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji. 18#Kut 24:13; Mwa 41:38; Amu 3:10BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu mwenye roho ndani yake, ukamwekee mkono wako; 19#Kum 31:7kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; ukampe mausia mbele ya macho yao. 20#Hes 11:17; 1 Sam 10:6; 2 Fal 2:15; Kum 34:9; Yos 1:15Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii. 21#Kut 28:30; 1 Sam 14:41; 28:6; Yos 9:14; Amu 1:1; 20:18; 1 Sam 23:9; 30:7; Law 8:8; Kum 33:8; 1 Sam 28:6; 1 Sam 22:10Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia. 22Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; 23#Kum 3:28; 31:23; Isa 55:4kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa.
Iliyochaguliwa sasa
Hes 27: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.