Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nah 3

3
Kuja kwa Uharibifu Usioepukika
1Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi; mateka hayaondoki. 2Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; 3mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. 4#Isa 47:9; 2 The 2:9,10; Dan 2:2; Ufu 9:20,21Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.
5 # Isa 47:2,3 Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako. 6Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau. 7Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji?
8Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake. 9#Eze 30:5Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Putu na Walibia walikuwa wasaidizi wake. 10#Yoe 3:3; Oba 1:11Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo. 11Tena utalewa, utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui. 12#Ufu 6:13Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye. 13#Isa 19:16; Yer 50:37Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako.
14Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako;
Zitie nguvu ngome zako;
Ingia katika udongo, yakanyage matope,
Itie nguvu tanuru ya kuokea matofali.
15 # Yoe 1:4 Huko moto utakuteketeza;
Upanga utakukatilia mbali;
Utakumeza kama tunutu alavyo;
Jifanye kuwa wengi kama tunutu!
Jifanye kuwa wengi kama nzige!
16Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake. 17#Ufu 9:7Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani.
18 # Yer 50:18; Eze 31:3; 1 Fal 22:17 Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya. 19#Isa 14:8; Omb 2:15; Sef 2:15Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima?

Iliyochaguliwa sasa

Nah 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia