Omb 3:17-24
Omb 3:17-24 SUV
Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.