Maombolezo 3:17-24
Maombolezo 3:17-24 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Amani yangu imeondolewa, nimesahau kufanikiwa ni nini. Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo. Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu. Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Nimeiambia nafsi yangu, “Mwenyezi Mungu ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.”
Maombolezo 3:17-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Moyo wangu haujui tena amani, kwangu furaha ni kitu kigeni. Nimewaza “Nimekata tamaa kabisa, tumaini langu kwa Mwenyezi-Mungu limetoweka.” Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangu kwanipa uchungu kama wa nyongo. Nayafikiria hayo daima, nayo roho yangu imejaa majonzi. Lakini nakumbuka jambo hili moja, nami ninalo tumaini: Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Mwenyezi-Mungu ndiye hazina yangu hivyo nitamwekea tumaini langu.
Maombolezo 3:17-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
Maombolezo 3:17-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA. Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.