Ayu 32:15-22
Ayu 32:15-22 SUV
Wameshangaa, hawajibu tena; Hawana neno la kusema. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena; Mimi nami nitajibu sehemu yangu, Mimi nami nitaonyesha nionavyo. Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya li karibu na kupasuka. Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote. Kwani mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.