Yobu 32:15-22
Yobu 32:15-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wameshangaa, hawajibu tena; Hawana neno la kusema. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena; Mimi nami nitajibu sehemu yangu, Mimi nami nitaonyesha nionavyo. Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya li karibu na kupasuka. Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote. Kwani mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.
Yobu 32:15-22 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nyinyi mmeduwaa; mmeshindwa, nyinyi hamna cha kusema zaidi. Je, ningoje tu kwa vile hamsemi, kwa sababu mnakaa tu bila kujibu kitu? Mimi pia nitatoa jibu langu; mimi nitatoa pia maoni yangu. Ninayo maneno mengi sana, roho yangu yanisukuma kusema. Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka. Ni lazima niseme ili nipate nafuu; yanipasa kufungua kinywa changu na kujibu. Sitampendelea mtu yeyote wala kutumia maneno ya kubembeleza mtu. Maana mimi sijui kubembeleza mtu, la sivyo, Muumba wangu angeniangamiza.
Yobu 32:15-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wameshangaa, hawajibu tena; Hawana neno la kusema. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena; Mimi nami nitajibu sehemu yangu, Mimi nami nitaonesha nionavyo. Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya liko karibu kupasuka. Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote. Kwa kuwa mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.
Yobu 32:15-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema; maneno yamewaishia. Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya, kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu? Mimi nami nitakuwa na la kusema; mimi nami nitasema lile nilijualo. Kwa kuwa nimejawa na maneno, nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma; ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka. Ni lazima niseme ili niweze kutulia; ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu. Sitampendelea mtu yeyote, wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote; kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza, Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.