Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Gal UTANGULIZI

UTANGULIZI
Paulo aliandika waraka huu baada ya safari yake ya kwanza ya kitume na kuanzisha makanisa sehemu ya kusini mkoani Galatia. Sehemu hiyo sasa ni Uturuki. Makanisa yaliyoanzishwa mkoani humo ni ya miji ya Antiokia, Ikonio, Listra ambapo ni nyumbani kwa Timotheo, na Derbe (Mdo 13:13–14:23). Paulo alifanya ziara zaidi ya mbili katika Mkoa wa Galatia (Mdo 16:6; 18:23).
Baada ya Paulo kutoka Galatia, baadhi ya Wakristo wa Kiyahudi walifika huko wakafundisha kwamba ili Wakristo wakamilike katika wokovu hawana budi kufuata mila, desturi na sheria za dini ya Kiyahudi. Walidai kuwa ili mtu apate kuokolewa anapaswa kutahiriwa na kushika Torati ya Musa eti kwa sababu imani na ubatizo katika Yesu Kristo havitoshi. Walipinga na kupuuza mafundisho ya Paulo. Wakamdhalilisha kwa kusema kwamba Paulo sio mtume ila alipata mafundisho machache kutoka kwa Petro na Yakobo. Wagalatia walivutwa na mafundisho hayo wakaanza kuyaamini na kuyafuata (1:6; 4:10). Madai hayo ndiyo ajenda ya Mkutano wa Kanisa hapo Yerusalemu (Mdo 15).
Paulo aliandika Waraka huu kukanusha madai ya kikundi cha Wayahudi hao, na kukemea walioanza kupokea mafundisho mapotovu ya kikundi hicho. Anaeleza kuwa yeye ni mtume halisi. Utume wake na Injili aihubiriyo amevipokea kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe na sio kutoka kwa mtu (1:13-2:21). Paulo anatetea “kuhesabiwa haki kwa imani na kuwa huru kutoka sheria”. Wokovu haupatikani kwa sheria bali kwa neema ya Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo (1:7; 2:16). Paulo anatoa mfano wa Abrahamu aliyeishi kabla ya kuwekwa Torati ya Musa jinsi alivyohesabiwa haki kwa imani. Torati ya Musa ni kama mlezi aliyeongoza ili kufikia wokovu mkamilifu uliotolewa na Yesu Kristo. Wakristo ni wana wa Mungu kwa imani katika Yesu Kristo (3:7). Kristo aliondoa utumwa wa sheria akatangaza uhuru. Hivyo uhuru huu utumiwe kwa kumtii Roho Mtakatifu (5:16) na kuzaa matunda yampendezayo Mungu (5:14).

Iliyochaguliwa sasa

Gal UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha