Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Kor 13

13
Maonyo Zaidi
1 # Kum 17:6; 19:15; Mt 18:16; 1 Tim 5:19 Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. 2Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia; 3kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu. 4#Flp 2:7,8Maana, alisulibiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu. 5#1 Kor 11:28Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 6Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. 7Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa. 8#1 Kor 13:6Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. 9Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu. 10#2 Kor 2:3; 10:8,11Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Salamu za Mwisho na Baraka
11 # Flp 4:4; Rum 15:33 Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12#1 Kor 16:20Salimianeni kwa busu takatifu. 13Watakatifu wote wawasalimu.
14Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Iliyochaguliwa sasa

2 Kor 13: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia