Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 12

12
1Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.
2Kabla jua, na nuru, na mwezi,
Na nyota, havijatiwa giza;
Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
3 # Zab 71:9; Zek 8:4; 2 Kor 5:1; Mwa 27:1 Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetema;
Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha;
Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba;
Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
4 # Mik 7:1; 2 Sam 19:35 Na milango kufungwa katika njia kuu;
Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo;
Na mtu kusituka kwa sauti ya ndege;
Nao binti za kuimba watapunguzwa;
5 # Law 19:32 Naam, wataogopa kilichoinuka
Na vitisho vitakuwapo njiani;
Na mlozi utachanua maua;
Na panzi atakuwa ni mzigo mzito;
Na pilipili hoho itapasuka;
Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele,
Nao waombolezao wazunguka njiani.
6Kabla haijakatika kamba ya fedha;
Au kuvunjwa bakuli la dhahabu;
Au mtungi kuvunjika kisimani;
Au gurudumu kuvunjika birikani;
7 # Mwa 3:19; Mhu 3:21; Mwa 2:7; Hes 16:22 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
8Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!
Hitimisho
9Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi. 10Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli. 11Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja. 12Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
13Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;
Mche Mungu, nawe uzishike amri zake,
Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
14 # Mt 12:36 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 12: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia