Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 11

11
Thamani ya kuwa na Bidii
1 # Kum 15:10; Mit 11:18; Mt 10:42; 2 Kor 9:6 Tupa chakula chako usoni pa maji;
Maana utakiona baada ya siku nyingi.
2 # Zab 112:9; Lk 6:30; Mik 5:5; Efe 5:16 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane;
Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.
3Mawingu yakiwa yamejaa mvua,
Yataimimina juu ya nchi;
Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini,
Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.
4Mwenye kuuangalia upepo hatapanda;
Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
5 # Yn 3:8 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
6Asubuhi panda mbegu zako,
Wala jioni usiuzuie mkono wako.
Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Ujana na Uzee
7Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. 8Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. 9#Kum 29:19; Zab 81:12; Mdo 14:16; Efe 2:2,3; Mhu 12:14; Rum 2:6Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. 10#2 Kor 7:1Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 11: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia